https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Monday, October 17, 2016

Jkt watoa taarifa kuhusu utapeli unaoendelea ili kujiunga na jeshi la kujenga taifa

Leo October 17, 2016 Nimeipata hii kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu kuutaarifu umma juu ya utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kupatiwa malipo.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT imeelezwa kuwa utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.

Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT hutolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.

Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>