https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Thursday, November 17, 2016

Raymond atuhumiwa kuiba baadhi ya mistari kwenye wimbo wa msanii wa Singeli


Msanii wa WCB, Raymond anatuhumiwa kutumia baadhi ya mistari ya wimbo wa msanii wa muziki wa Singeli, Manyo Lee kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sugu’.
raymond

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Manyo Lee amesema, “Mimi nilisikia kwa watu tu kuwa dogo kachukuwa mashairi yangu. Juzi kati lilifanyika tamasha kubwa tu nikaona akiimba yale mashairi lakini nikaona kawaida tu lakini hivi karibuni nimeona kaachia video kabisa nikaona kumbe dogo yupo serious kabisa.”
“Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu funga virago shetani. Joh Makini akiwa mweusi Barakah tumuite nani?,” mistari ambayo Raymond anadaiwa kuchukua kwenye wimbo wa msanii huyo unaoitwa ‘Mwendo wa Pushapu’.
Naye Manyo Lee katika wimbo wake aliouachia mwezi Septemba mwaka huu ameimba, “Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu virago funga shetani. Makini ajiite mweusi na Nigga ajiite nani?.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>