https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Tuesday, October 11, 2016

Wanafunzi watembea kilomita 13



File Photo

Tarime. Wakazi wa Kijiji cha Nyakunguru wilayani hapa wameitaka Serikali kuifungua Shule ya Sekondari ya Genge ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.
Shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Mgodi wa North Mara.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abel Maginga amesema hivi sasa wanafunzi wanaotoka vijiji vya Nyakunguru na Nyamichele wanatembea umbali wa kilomita 13 kwenda Shule ya Sekondari ya Kata ya Kisabasuka.
Sekondari ya Genge ina madarasa manne, nyumba tatu za walimu, jengo la utawala, matundu 10 ya vyoo na tangi la kuvuna maji ya mvua. Ujenzi umegharimu Sh564 milioni.
Diwani wa kata hiyo, Loyce Manyata amesema ili mwanafunzi awahi vipindi vya kwanza ni lazima aamke saa 10:00 usiku na iwapo akiamka saa 12:00 asubuhi atafika shuleni saa 2:00 asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga aliagiza sekta ya elimu wilayani hapa kupeleka walimu kwenye shule hiyo na kuwagawa wanafunzi wa sekondari za Kibasuka wanaotoka vijiji vya Nyakunguru na Nyamichere ili wahamie kwenye shule hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Emmanuel Jonson aliahidi kuhakikisha shule hiyo inafunguliwa kwa kuwa imekidhi vigezo vinavyotakiwa.

mwananchi
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>