Mchekeshaji maarufu wa Marekani, Kevin Hart amefanikiwa kuungana na mastaa wengine duniani waliowahi kupatiwa heshima ya nyota ya Hollywood Walk of Fame.
Kupata heshima ya nyota hiyo ni ndoto ya kila staa duniani kwa kuwa si kila mtu anaweza kupata nafasi hiyo. “You can’t do it by yourself….you need a team that believes in you & in your vision. I have that in my friends/brothers…. We are more focused now than we have ever been,” ameandika Kevin kwenye moja ya picha aliyoweka kwenye mtandao wake wa Instagram.
Mastaa wengine waliowahi kupatiwa heshima kama hiyo ni pamoja na Shirley Caesar, Clarence Avant, Michael Jackson, Paula Abdul, Madonna, Beyonce, Celine Dion, na wengine.
Siku chache zilizopita jarida la Forbes lilimtangaza Kevin Hart kuwa ndiye anayeongoza orodha ya wachekeshaji waliolipwa fedha nyingi kuanzia mwezi Juni mwaka jana akiwa ameingiza kiasi cha $87.5 milioni.
0 comments:
Post a Comment