Baada
ya agizo la Rais John Magufuli kuwataka watumishi wote waliopewa posho
za kuhudhuria kilele cha mbio za Mwenge, Madereva na Wasaidizi wa Wakuu
wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali nchini ambao walikuwa tayari
wamefika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe hizo wameeleza kuumizwa na
agizo la kurejesha fedha za kujikimu ambazo kiasi walizitumia kwa
shughuli husika.
Rais wa Zanzibar Dr. Shein akihutubia maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Madereva
na wasaidizi hao wamedai agizo hilo lilitolewa na Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli limewatengenezea tatizo la kiuchumi baada ya kuwafikia kwa
kuchelewa huku baadhi yao wakidai kuwa hawana uwezo wa kurejesha fedha
hizo kwasababu hawakuomba kufanya safari hizo bali ilikuwa sehemu ya
kazi zao na kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na
ofisi kuwawezesha kufika na kuishi katika eneo hilo.
>>>Sisi
hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa
mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwa sababu ilibidi tule na kulala
kwenye nyumba za wageni. Hapo sisi kosa letu liko wapi:- Dereva
>>>Ilinibidi
nimlipe mwenye chumba gharama zote za siku 7 ambazo nilitarajiwa kuishi
hapa kama nilivyotumwa kwasababu ya uhaba wa vyumba. Sasa naanzaje
kumwambia mwenye hotel anirudishie pesa yangu yote ili nirejeshe
ofisini?:- Msaidizi wa mkuu wa mkoa
Hata
hivyo, wakati wasaidizi wa viongozi hao wakionesha kuvurugwa na agizo
hilo ambalo wanasema limewaingiza hasara ambayo imetokana na kutumwa
wafanye wajibu wao, baadhi ya wakuu wa mikoa tayari wameshaanza
kurejesha fedha hizo.
Hivi
karibuni Rais Magufuli aliagiza viongozi wote pamoja na wasaidizi wao
waliokuwa wamepanga kuhudhuria sherehe za kuzimwa Mwenge Mkoani Simiyu
zilizofanyika siku ya Ijumaa, wasitishe safari zao na waliochukua posho
wazirejeshe.
0 comments:
Post a Comment