https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Tuesday, October 11, 2016

Shahidi kortini kwa saa 3 kesi ya bilioni saba

 
SHAHIDI wa tatu, Fredrick Umio (43), katika kesi ya wizi, kughushi na kutakatisha fedha zaidi ya Sh bilioni saba ameieleza Mahakama kuwa alipokabidhiwa ofisi aliambiwa baadhi ya nyaraka zimeharibiwa na hazipo katika chumba maalumu cha kuhifadhi nyaraka.
Kesi hiyo inawakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa Benki ya Exim, tawi la Arusha na mfanyabiashara. Umio, Meneja Mkuu wa benki hiyo, ametoa ushahidi kwa siku nne tofauti.

Aliwahi kutoa ushahidi awali na kurudishwa tena kutoa ushahidi kwa mujibu wa sheria. Amesema, alikabidhiwa ofisi na Meneja wa wakati huo aliyatambuliwa kwa jina la Hamad Said.
Shahidi huyo alisema hayo wakati akihojiwa na wakili wa washtakiwa, Philipo Mushi na kusema kuwa taarifa hiyo haikuwa kwenye maandishi, bali alielezwa kwa mdomo.
Alidai wakati tukio la wizi linatokea yeye hakuwa meneja wa benki hiyo mwaka 2011/12 ila alikuta upelelezi wa kesi hiyo ukiendelea na alikuwa akitoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Arusha, Idara ya Upelelezi na Makosa ya Jinai.
Umio alidai ameruhusiwa kuja kutoa ushahidi na viongozi wake wa juu ya Benki ya Exim na amekuja kutoa ushahidi kwa vitu vilivyo ndani ya uwezo wake vya kitaalamu na si vinginevyo kwa sababu yeye si msemaji wa benki hiyo.
Amedai hana uhakika kama Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ililipwa fedha zake zaidi ya dola za Marekani 790,000 zilizoibwa kwa kuwa yeye si msemaji wala si mhusika wa kujua hilo.
Shahidi huyo alikuwa akitoa ushahidi kwa saa tatu mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha na Arumeru, Deusdedit Kamugisha na alidai kuwa alikuwa akihojiwa na Polisi kama Meneja wa tawi la Arusha na kutoa nyaraka za kibenki kwa maandishi pindi anapohitajika kufanya hivyo.
Alipoulizwa na wakili Mushi kama benki hiyo iliwahi kupata hasara katika miaka ya 2011/12 alisema hawezi kujua, ila ukaguzi hufanyika kila mwaka kwa mujibu wa utaratibu wa kibenki na hukaguliwa na wakaguzi wa ndani, wakaguzi wa nje na ukaguzi wa Benki Kuu.
Shahidi huyo pia amedai mahakamani kuwa kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu upoteaji wa fedha katika akaunti za wateja, kwani baadhi yao walilalamika kwa maandishi na malalamiko hayo yako ofisini.
Wafanyakazi hao ni pamoja na aliyekuwa Meneja wa Benki tawi la Exim Arusha, Bimel Gondalia (37), Lilian Mgaya (33), Livingstone Julius (36) Joyce Kimaro (36), Daud Mosha, Doroth Tigana (50), Evans Kashebo (40), Tuntufye Aggrey (32), Joseph Meck (34), Jane Massawe (32), Christopher Lyimo (34) na mfanyabishara wa Arusha, Gervas Hugo.
Washitakiwa wawili, Neema Kinabo (30) na Mosses Chacha (37) waliachiwa baada ya kukiri kosa na kulipa faini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>