Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford yupo kwenye kinyang’anyiro cha kushinda tuzo ya Golden Boy kwa mwaka 2016 hiyo imetokana na kiwango bora alichoonesha kwa klabu yake katika mwaka huu.
Baadhi ya wachezaji wanaoshindana na Rashford katika tuzo hiyo ni kinda wa Arsenal, Alex Iwobi, kiungo wa Tottenham Hotspur, Dele Alli, wachezaji wawili wa Bayern Munich, Kingsley Coman na Renato Sanches, wengine wawili kutoka Manchester City, Kelechi Iheanacho na Leroy Sane, chipukizi wa Liverpool, Marko Grujic na winga machachari wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele.
Rashford, 18, amefunga magoli nane katika michezo 15 ya Ligi Kuu tangu alipocheza kwa mara ya kwanza February mwaka huu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ni moja ya majina 40 yanayowania tuzo hiyo ya Golden Boy, ambayo ilianzishwa mwaka 2003 na Tuttosport, inapigiwa kura na waandishi wa habari kutoka katika magazeti 30 ya Ulaya. Washindani wote lazima wawe chini ya miaka 21, wanacheza katika ligi ya daraja la juu zaidi katika nchi ya Ulaya pia washindani wote ni lazima wawe hawajawahi kushinda tuzo hiyo hapo kabla.
Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial alishinda tuzo hii mwaka jana (2015), wakati washindi wa hapo nyuma wakiwa ni Raheem Sterling (2014), Paul Pogba (2013), Mario Balotelli (2010) na Lionel Messi (2005)
Kocha wa Celtic, Brendan Rodgers alisema hashangazwi na kujumuishwa kwa mshambuliaji wake, Moussa Dembele – ambaye yupo kwenye kiwango cha juu sana kwa sasa – kwa kuwa anastahili.
“Ni uteuzi wa haki” alisema Rodgers. “Ni mchezaji mdogo (kiumri) mwenye kipaji kikubwa na uzuri wa Moussa ni kuwa anapenda kuendelea. Nadhani bado anaweza. Ana kipaji kikubwa na alikuwa tishio sana kwenye mechi dhidi ya Manchester City, alifunga goli mbili katika sare ya 3-3 – anastahili sana kuwemo.
0 comments:
Post a Comment