Matumaini ya kina dada Chelsea
kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya yamefifia baada yao kulazwa 3-0 na
kina dada wa Wolfsburg uwanjani Stamford Bridge.
Chelsea, ambao kwa sasa wanaongoza ligi kuu ya kina dada Uingereza, walionekana kulemewa kipindi chote cha mechi hiyo iliyotazamwa na mashabiki 3,783.
Wolfsburg, waliofika fainali msimu uliopita, watakuwa wenyeji mechi ya marudiano tarehe 12 Oktoba.
Klabu hiyo imetwaa ubingwa mara mbili tangu msimu wa 2012-13.
Chelsea walishindwa kwa jumla ya mabao 4-1 na Wolfsburg hatua ya klabu 16 bora msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment