https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Friday, October 28, 2016

Rais wa Ufilipino adai amesikia sauti ya Mungu

Rais Rodrigo Duterte wa ufilipino
Rais Rodrigo Duterte wa ufilipino

RODRIGO Duterte, Rais wa Ufilipino ambaye siku chache zilizopita alisema hahitaji kuongozwa kama mbwa na taifa la Marekani, amesema ataacha matusi kwani amesikia Sauti ya Mungu ikimuonya, anaandika Wolfram Mwalongo.

Duterte amesema alipokuwa akirejea kutoka ziarani nchini Japan, akiwa kwenye ndege na abiria wengine wakiwa wamelala alisikia sauti ikimuonya na kumtishia kuiangusha ndege yake.
“Nilisikia sauti hiyo ikisema, usipokoma nitaangusha ndege hii, nikajua sauti hiyo ilikuwa ni ya Mungu,” amesema Duterte.
Kiongozi huyo maarufu kwa lugha ya matusi na maneno ya kashfa hasa dhidi ya viongozi wa mataifa mengine duniani, amesema ataacha tabia hiyo kufuatia onyo alilolipata kupitia sauti hiyo.
Itakumbukwa kuwa mara ya mwisho Duterte alimtusi Barack Obama Rais wa Marekani kwamba ni “mwana wa kahaba”, alimtukana pia John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani huku akimwambia Philip Goldberg, balozi wa Marekani nchini Ufilipino kuwa ni shoga.
Akihutubia wananchi wa jiji la Davao mahali ambapo alihudumu katika nafasi ya Meya kwa miaka 22 na kujipatia umaarufu kutokana na kupambana na walanguzi wa mihadarati ameongeza kuwa ahadi kwa Mungu ni sawa na ahadi kwa Wafilipino.
Mtazamo mpya wa Duterte umeibua mijadala katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya taifa hilo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>