Licha ya uongozi wa Mwadui FC kumkatalia kocha wao Jamhuri Kihwelu Julio kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, Julio bado ameendelea kushikilia msimamo wake kwamba hatoendelea kufundisha soka la Bongo na hatobadilisha uamuzi wake.
“Maamuzi yangu nimesema naondoka, siwezi kubaki nafsi yangu imeshakataa lakini kwa wakati huu mimi naondoka,” anasisitiza Julio.
“Bado sijaondoka kwasababu uongozi wangu wa juu haukuwa tayari mimi kufanya hivyo lakinin kama wangekuwa tayari, ningepata stahiki zangu ili niondoke lakini nao bado hawataki kukubaliana na mimi.”
Julio alitangaza kustaafu kufundisha soka Tanzania mara baada ya timu yake kuchapwa 1-0 na Mbeya City huku akitaja tatizo la waamuzi kutotenda haki ni sababu kubwa ya yeye kuamua kukaa pembeni.
0 comments:
Post a Comment