https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Wednesday, October 19, 2016

Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara (VPL), itaendelea leo Jumatano Oktoba 19

Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), itaendelea leo Jumatano Oktoba 19, mwaka huu wakati kesho Alhamisi Oktoba 20, kutakuwa na mchezo mmoja tu.
football-2

VPL, leo patakuwa na michezo ya Ruvu Shooting ya Pwani ambayo itaikaribisha Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Mabatini uliuoko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo Na. 81 wa VPL utakaoanza saa 10.00 jioni.
Mchezo Na. 82 utakaozikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro utafanyika saa 1.00 usiku (19h00). Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – maskani ya Azam yalioko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati mchezo Na. 83 utazikutanisha timu za Ndanda FC na Mbeya City ya Mbeya kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mchezo Na. 85 utazikutanisha timu za Tanzania Prisons ya Mbeya na Stand United itakayokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku mechi Na. 87 itazikutanisha Toto African ya Mwanza itakayocheza na Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati African Lyon itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwenye mchezo Na. 88.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamisi Oktoba 20, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako vinara wa ligi hiyo kwenye msimamo hadi sasa, Simba itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza katika mchezo Na. 84.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>