https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Monday, October 10, 2016

Amber lulu aongea haya kuhusu uvumi wa kukamatwa kwake

Kufuatia madai ya kukamatwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ jijini Arusha kuelekea China, video queen matata Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefungukia ishu hiyo akidai kuwa anaamini ilitengenezwa na watu walioamua kumchafua.

Amber Lulu aliliambia Wikienda kuwa alishangaa kuona mitandaoni kwamba amekamatwa na unga, lakini hakuna kitu kama hicho kwani hajawahi kukamatwa.

Kabla ya kumpata Amber Lulu, simu yake ilikuwa haipatikani hivyo Wikienda lilimtafuta mdogo wake aliyeko jijini Mbeya ambaye naye alikiri kutompata mrembo huyo hewani kwa siku tatu ambapo ndugu walimtafuta kwenye vituo vya polisi jijini Arusha bila mafanikio.

Wapo baadhi ya watu waliodai kuwa ni kiki iliyofanywa na Amber Lulu mwenyewe ili kuwafanya watu wamuongelee



Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>