https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Monday, November 7, 2016

Askofu- Mafataki acheni kuoa wanafunzi

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, John Ndimbo ameitaka Serikali ya Awamu ya Tano kutokuwa na huruma kwa wanaume wanaokatisha masomo ya watoto wa kike waliopo mashuleni kwa kuwapa mimba na wengine kudiriki kuwaoa. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kuna wanawake wengi watu wazima wanaohitaji watoto.
Amesema vitendo hivyo, licha ya kuwa havimpendezi Mungu na vimekuwa vikikatisha ndoto za wasichana wengi hapa nchini na kurudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike ambao nao wana haki ya kupata elimu sawa kama ilivyo kwa watoto wa kiume.

Askofu Ndimbo alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na madiwani, watumishi na baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kilichofanyika mjini hapa.
Alisema baadhi ya wanaume tena wengine wenye umri mkubwa, wakiwemo walimu wamekuwa na tabia mbaya ya kufanya mapenzi na wasichana ambao bado wako shuleni, jambo ambalo limekuwa likikatisha ndoto na matumaini ya wasichana wengi katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, ameishauri serikali kupitia halmashauri ya wilaya kuiangalia kwa jicho la huruma Shule ya Msingi Kitulo ambayo ina hali mbaya kwa kuta zake kuwa na nyufa, kukosa milango, madirisha, na walimu kukosa sehemu ofisi zenye hadhi kama ilivyo kazi zao ambazo zingewashawishi kufanya kazi zao kwa kujituma na moyo wa uzalendo.
Sambamba na hilo, Askofu Ndimbo alisema ni muhimu sana kwa serikali kufanya upendeleo wa kutenga kiasi cha fedha ili kuifanyia ukarabati shule hiyo ambapo hata walimu wake wameonekana kukata tamaa hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wao kikamilifu, jambo linaloweza kurudisha kiwango cha taaluma.
Pia Askofu Ndimbo ameomba kupelekwa kwa walimu wa kike ili wawasaidie wanafunzi wa kike pale inapotokea dharura ya kimaumbile ili kuwatendea haki, kwani inakuwa vigumu kupata msaada hata wa ushauri kutoka kwa mwalimu wa kiume.
Hata hivyo, amewapongeza watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo namna wanavyoendesha vikao vyao kwa umakini mkubwa katika kupanga na kutekeleza miradi mingi ya maendeleo yenye lengo la kupunguza kero zinazowakabili wananchi.


Amewasihi kuendelea na umoja wao, kushirikiana na kuvumiliana na kufanya kazi pamoja kama mchwa na kuweka kando tofauti zao za vyama, hatua itayaosawaidia kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo katika kata zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>