Kawaida taifa linaloongoza kwa teknolojia ya
angani yaani mifumo ya kisasa ya RADA na
ndege vita huongoza kwa nguvu za kijeshi. pia
idadi ya askari ambao wana silaha nzito nzito
huongeza kigezo. meli za kisasa zenye nguvu na
nyambizi(submarine), makombora ya masafa
marefu na ysle ya kudungua ndege au
makombora ya kudungua makombora mengine,
vifaru vingi vya kisasa na magari yenye vifaa
maalum ya kivita huongeza 'credit'. mbinu na
uzoefu wa kupigana vita nyingi na hasa ngumu
pia ni kigezo. Mataifa yafuatayo yanafunika ktk
hayo:
1. MAREKANI. hawa wanaongoza kwa
kutengeneza na kuuza ndege nyingi za kisasa na
hatari sana duniani mfano B-2 SPIRIT
isiyoonekana kirahisi kwenye rada, F-16 n.k.
ndege zao zimeuzwa hadi Italy, Israel na Saudi
Arabia. Pia uwezo wao wa kupambana na adui
yeyote huwapa maksi kubwa. Aircraft carrier
walizonazo, zimewapa maksi kubwa. pia
wanasifika kuwa na vikosi hatari vya
makomandoo vijulikanavyo kama SEAL-SEA, AIR
and LAND
2. URUSI: wako vizuri ila kusambaratika kwa
USSR kuliwafanya washuke kiuchumi na hivyo
uwezo wao wa kijeshi kidogo ukaathiriwa. hili
ndo taifa lenye ndege nzuri nyingi za kisasa
baada ya Marekani. mataifa mengi
yasiyoshibana na nchi za magharibi hupenda
kununua ndegevita na vifaa vingine hatari kwa
Warusi. mfano IRAN, SYRIA na LIBYA
3. CHINA: wako vizuri pia hasa ardhini na majini.
ndegevita zao havina nguvu sana ukilinganisha
na zile za Wamarekani na Warusi.
wanatengeneza makombora mazuri na hatari
sana. wana vifaa vingi vikali vya jeshi la ardhi
hasa vifaru imara na vya kisasa. wanaongoza
kuwa na idadi kubwa ya askari duniani tena
wakiwa na silaha nzitonzito.
4. UINGEREZA: wapo vizuri pia hasa angani na
pekee sana majini. ndege zao maarufu za kivita
ziitwazo PHANTOM zinawabeba sana. wanasifika
kuwa na mimeli na minyambizi ya hatari.
5. JAPAN: wazuri na wasiri sana ktk teknolojia
zao za kivita. ktk mataifa makubwa duniani
Japan hawapendi kuuza sana silaha zao za
kivita. ndiyo sababu ktk vita ya dunia kambi za
kijeshi za Marekani zilipigwa na ndegevita hatari
za Kijapan ambazo Wamarekani hawakuwahi
kuzijua. waliwajibu kwa NYUKLIA huko
HIROSHIMA na NAGASAKI. cha pekee kwa
Wajapani ni mimeli ya kisasa. najua mnafahamu
viwanda vikubwa duniani vya meli viko huko. pia
jeshi lao la ardhi liko vizuri sana.
Nimeipenda hii
ReplyDelete