Michelle Obama
Wasichana 25 wa Tanzania wanatarajiwa kufanya majadiliano ya moja kwa moja na mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama wiki ijayo.
Wasichana hao ni miongoni mwa wasichana wa nchi tatu watakaoshiriki majadiliano hayo yenye lengo la kumuwezesha mtoto msichana katika masuala mbalimbali na upatikanaji wa fursa.
Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen amesema nchi nyingine zitakazoshiriki katika majadiliano na mke wa Obama ni Peru na Cambodia.
Alisema katika kuadhimisha siku hiyo, wadau wataombwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kundi hilo na kupewa nafasi ya kujifunza, kuongoza, kuamua na kuishi ili kuonesha thamani ya mtoto wa kike na hata kwa kuwapa fursa sawa.
Alisema watoto wa kike wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na vikwazo kuanzia katika jamii, ambapo pindi wakiaminiwa wanaweza kufanya mambo mbalimbali katika eneo la kisiasa, kiuchumi na hata kijamii.
0 comments:
Post a Comment