https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Wednesday, October 12, 2016

Theo Walcott na ubinafsi wa Sturridge wainyima ushindi England

sturridge
Haijalishi ni ubovu kiasi gani waliouonesha kwenye michuano ya Euro 2016, ni ngumu kuamini England wangetoka uwanjani vichwa chini baada ya pambano dhidi ya Slovenia.
Wakiwa chini ya kocha wa muda Gareth Southgate, England walitawaliwa na wenyeji wao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo na ilikuwa ni bahati kwao kupata ugenini.


Theo Walcott bado ameshindwa kuonesha makali yake kwenye michezo miwili ya kimataifa licha ya kupewa nafasi kwenye timu ya taifa.
Anaonekana kukosa makali na ilibidi atolewe kipindi cha pili akiwa hajafanya chochote cha maana uwanjani.
Daniel Sturridge ni mchezaji mwingine ambaye ameonesha kiwango duni wakati wa mchezo huo.
Striker huyo wa Liverpool hakuonesha kitendo chenye picha nzuri kutokana na kuwa mbinafsi kwa kushindwa kutoa pasi ambazo pengine zingezaa magoli.
Akionekana hana mpango kabisa na wachezaji wenzake, Sturridge aliendelea na vitendo vyake vya kucheza kwa ubinafsi na kushuhudiwa baadaye akitolewakumpisha Rashford.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>