Inawezekana Nkongo alimsikia mtangazaji huyo, katika ukurasa wake rasmi wa facebook, mwamuzi huyo mkongwe wa kimataifa ame-post raba ambazo alitumia kuchezesha mchezo huo na kuuliza swali kwa namna ya kumjibu mwandishi huyo.
Ujumbe huo unasomeka hivi: “Eti ni kituko mwamuzi kuvaa viatu visivyo na njumu wakati anachezesha mpira. SHERIA namba ngapi????” amehoji Nkongo kupitia ukurasa wake wa facebook ambapo ame-post pia picha ya viatu alivyovitumia wakati akichezesha mchezo husika.
Kumbuka uwanja wa Uhuru ulishalalamikiwa na vilabu vya Simba na Yanga kwamba, hauko katika ubora wa kuchezewa mechi za ligi kwasababu tangu ulivyowekwa nyasi za bandia haukutumika kwa muda mrefu na kusababisha kuwa mgumu.
Tayari kuna baadhi ya wachezaji walishapata majeraha kutokana na ubovu kama si uchakavu wa uwanja wa Uhuru hasa katika eneo la kuchezea (pitch).
Simlaumu Nkongo kuamua kuvaa raba za kawaida na si viatu vyenye njumu, uwanja ukiwa mgumu unawasababishia wachezaji au waamuzi maumivu ya nyama na mifupa kendapo watavaa viatu vyenye meno (njumu).
Ukiangalia kwa makini raba alizovaa Nkongo wakati akichezesha mchezo kati ya Azam na Yanga utagundua raba hizo zina soli nene, hii ni kwa ajili ya kupunguza maumivu ya nyama na mifupa ambayo yangekuwa makubwa endapo angevaa viatu vyenye njumu.
Ikumbukwe serikali iliviruhusu vilabu vinavyoutumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani kuutumia uwanja wa taifa baada ya kupeleka malalamiko ya ubovu wa uwanja wa Uhuru ambao unahatarisha usalama wa wachezaji. Lakini baada ya uharibifu uliotokea siku ya mechi ya watani wa jadi Yanga vs Simba, serikali ikatangaza kuufunga uwanja huo.
Kwahiyo vilabu vya Simba, Yanga na African Lyon vinalazimka kuutumia uwanja wa Uhuru licha ya awali kuupiga vita kutokana na ubovu wake.
0 comments:
Post a Comment