October 12, 2016 Kenya
inaingia kwenye headlines tena ikiwa ni baada ya mwimbaji staa wa
Marekani Chris Brown kufanya show weekend iliyopita Mombasa, mpya ya leo
imetoka kwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye inaelezwa ndiye alidhamini tamasha la Mombasa Rocks Music Festival.
Gavana wa Mombasa, Joho Mohamed
Story
kutoka 254 Kenya zinasema Gavana huyu inayedaiwa ana pesa za kutosha,
ametangaza kuwa timu yake imeanza mazungumzo na uongozi wa rapper Nicki Minaj ili aje Mombasa kutumbuiza hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Jamal Gaddafi aliyekua MC kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival amesema amepewa taarifa na Joho, awambie mashabiki wajiandae kwa show nyingine kubwa ya Nicki Minaj.
0 comments:
Post a Comment