Je! kiatu cha ufungaji bora msimu mpya ligi kuu bara kitaenda kwa mzawa au kitabaki kwa wageni kama msimu uliomalizika?
Pazia la ligi kuu Tanzania Bara lilifunguliwa agosti 20, ni msimu unaotarajiwa kuwa mgumu hasa kutokana na maandalizi mazuri kwa baadhi ya klabu Vita ya ufungaji msimu huu unatarajiwa kuwa wa upinzani mkubwa sana sababu kuu ni uwepo wa washambuliaji wapya  ligi kuu na wale wazamani kujiandaa vizuri
Msimu uliomalizika tuzo ya ufungaji bora ilikwenda kwa Mrundi Amis Tambwe baada ya kufunga goli 21, akifuatiwa na Hamis Kiiza goli 19, Donald Ngoma 17 na Jeremiah Juma 16
Je kiatu cha ufungaji bora msimu mpya ligi kuu bara kitaenda kwa mzawa au kitabaki kwa wageni kama msimu uliomalizika? Hii ni list ya washambuliaji 7 wenye nafasi ya kunyakua tuzo ya ufungaji bora kwa msimu wa 2016/2017
Amis Tambwe
 Image result for tambwe
Mrundi huyu mwenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli kwa stahili ya kichwa anatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa wa namba ndani ya kikosi cha Yanga baada ya ujio wa Obrey Chirwa, huyu ndiye mfungaji bora kwa msimu uliomalizika, anatazamiwa kutetea kiatu chake cha ufungaji bora kwa msimu mpya kama akiendelea kupata nafasi ndani ya timu yake
Laudit Mavugo
 Image result for mavugo simba
Mshambuliaji mpya wa Simba anatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwenye vita ya ufungaji bora kwa msimu mpya Tanzania bara  uwezo wake wa kufunga, nguvu alizo nazo  unatazamiwa kuwa changamoto kubwa sana kwa mabeki wa ligi kuu bara, alishafanikiwa kuwa mfungaji bora ligi kuu Burundi kwa vipindi tofauti tofauti
Donald Ngoma
 Image result for donald ngoma yanga
Msimu uliopita alimaliza na magoli 17 ligi kuu, alifanikiwa kutengeneza uwiano mzuri na Amis Tambwe kwa msimu uliomalizika, anatazamiwa kufunga magoli mengi msimu mpya hasa baada ya kuzoea mikiki-mikiki ya ligi kuu bara
Atupele Green

Image result for atupele green
Huyu ndiye mzawa anaye onekana mwenye nguvu ya kukimbazana na wageni kwenye kiatu cha ufungaji bora, mfungaji bora wa kombe la FA tayari amejiunga na JKT Ruvu akitokea ndanda ya Mtwara, anapewa nafasi kubwa ya kumaliza akiwa mfungaji bora kwa msimu mpya kama akipata ushirikiano mzuri ndani ya timu yake mpya
Jeremiah Juma
 Image result for jeremia juma
Amekuwa na msimu mzuri sana kwa miaka miwili iliyopita, msimu 2015/2016 alifanikiwa kumaliza na magoli 16 na ndiye mzawa pekee aliemaliza na idadi kubwa ya magoli kuliko wote, endapo akiendelea kujituma na kuaminiwa ndani ya timu yake anaweza kumaliza mmoja wa wafungaji bora kwa msimu mpya
Ibrahim Fofana
 Image result for IBRAHIM FOFANA AZAM FC
Mshambuliaji mpya wa Azam kutoka Ivory Coast, ana uzoefu wa kutosha kwenye mashindano makubwa ya Afrika, anapewa nafasi ya kuliziba vizuri pengo la Kipre pale Azam ambaye ametimkia Uarabuni
Ibrahim Ajib
 Image result for IBRAHIM AJIB
Uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kufunga ndio sababu ya wadau wengi kuamini msimu huu mshambuliaji huyu wa Simba anaweza kuwa mmoja wa wafungaji bora ligi kuu bara endapo akitumia nafasi vizuri anazopata uwanjani