https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Sunday, October 23, 2016

Mourinho alimnong’neza maneno haya Conte baada ya kipigo cha 4-0

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameonyesha kukerwa na namna meneja wa Chelsea Antonio Conte alivyoshangilia kwa kukera baada ya Chelsea kuiadhibu United mabao 4-0 jana.

Magoli kutoka kwa Pedro, Gary Cahill, Eden Hazard na N’Golo Kante yalileta maafa kwa Mourinho aliporejea kwa mara ya kwanza kabisa Stamford Brigde tangu alipotimuliwa mwaka jana.
Lakini licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, mashabiki wa United ndio walionekana kuwa na sauti zaidi hali iliyomsababisha Conte kuwaamsha mashabiki wake kuishangilia timu yao.
Kufuatia tukio hilo, baada ya mchezo Mourinho alimfuata Conte na kumkosoa kwa kitendo chake hicho.
“Usishangilie kwa namna hiyo ukiwa umeshinda 4-0, ingekuwa 1-0 sawa,lakini 4-0 inaumiza sana,” Mourinho alimwambia Conte maneno ambayo yalinaswa na vipaza sauti vilivyokuwa karibu.
Wakati alipoulizwa alimwambia nini Conte baada ya mchezo, Mourinho alikaa kujibu.
Kwa upande wake Conte alipoulizwa alitabasamu na kujibu: “Nadhani tuache mazungumzo binafasi yabaki kuwa binafsi, au sio.”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>