https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Thursday, October 20, 2016

List ya viwango vya ubora wa soka yatoka Tanzania yazidi kupotea

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina. Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu. Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne. Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi. Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107. Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138. Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32. Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24. Mataifa 10 bora duniani 1.Argentina 2.Ujerumani 3.Brazil 4.Ubelgiji 5.Colombia 6.Chile 7.Ufaransa 8.Ureno 9.Uruguay 10.Uhispania Mataifa 10 bora Afrika 31 Ivory Coast 32 Senegal 35 Algeria 38 Tunisia 45 Ghana 46 Misri 49 DR Congo 58 Mali 59 Cameroon
Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>