https://go.ad2upapp.com/afu.php?id=897810

KWA HABARI ZA KITAIFA KIMATAIFA MICHEZO MUZIKI BURUDANI NA AFYA KILA SIKU

Tuesday, October 11, 2016

Habari nzuri kanda ya ziwa Bakhresa kuingia kanda ya ziwa





File Photo

Dar es Salaam.  Kampuni ya Bakhresa Group imeeleza azma ya kuongeza viwanda vingine vya usindikaji matunda nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo,  Said Salim Bakhresa amesema ina mpango wa kujenga kiwanda kimoja mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 Amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam kwa ajili ya soko.
“Kuanzia Oktoba 15, tutaanza kupokea matunda kutoka Kahama na maeneo ya jirani, kwa siku tunapata zaidi ya semi trela 30. Yakimalizika ya kule, tunaanza kupokea mengine kutoka mikoa ya Pwani na Kusini,” amesema Bakhresa.
Amesema “Tukijenga kiwanda Kanda ya Ziwa, tutapunguza kero ya wadau kusafirisha matunda kutoka kule hadi hapa, badala yake tutakuwa tunasafirisha concentrated juice (juisi ghafi) na kuileta hapa kwa hatua zaidi za usindikaji.”
Amesema kampuni hiyo imeajiri zaidi ya wafanyakazi 8,000; wakiwamo Watanzania 180  waliopo kwenye matawi yake nje ya nchi.



Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

UNGANA NA SISI HAPO CHINI

Search This Blog

http://go.ad2upapp.com/afu.php?id=917347

Text Widget

Copyright © SAYARI 360 | Powered by Blogger

//]]>