10.Caracas,Venezuela
- Huu ni mji mkuu wa nchi ya Venezuela, Unatajwa kama mji ambao watalii wengi waliowahi kwenda huko kutoupenda kutokana na aina ya Uhalifu uliopo katika mji huo, Makundi ya wahalifu (Wauza Madawa ya Kulevya), Wezi, wakabaji, ni mambo ya kawaida ukiwa Venezuela.
9.Ciudad Juarez, Mexico
- Mexico inajulikana sana kwa usafirishaji wa biashara ya madawa ya Kulevya, moja kati ya miji inayoongoza kwa wasafirishaji wa madawa Ciuda Juarez nao umo, Ni mji wa matukio ya ajabu, risasi kusikika ni jambo la kawaida sana.
8.Cape Town, South Africa
- Huu ni moja kati ya miji inayopatikana kusini mwa Afrika katika nchi ya South Africa, Huu ni mji ambao umejaa matukio ya hatari sana duniani licha ya watalii wengi kwenda katika mji huu ila Ni hatari sana, Sababu nyingi zinasema ni Umaskini na matabaka yaliyopo South Afrika , na hali ya watu kumiliki silaha kirahisi husababisha kuwa moja kati ya miji ya kuogopwa
7. Rio De Janeiro
Huu ni mji uliopo Brazil, wengi tunaweza Tukaumbuka kutokana na matukio yaliyokuwa yakionekana kwenye michuano ya Olympics, Uporaji, Ukabaji, Milio ya Risasi ni kawaida sana uwapo Rio, Miji mingi ya Brazil imejaa wahalifu ila miaka ya karibuni Rio imeonekana kuwa juu zaidi ya miji hiyo kutokana na Wahalifu wengi wa miji mingine kukimbilia Rio. Kuna Beach nyingi za kuvutia ila Unaambiwa uendapo beach za Rio ni lazima uwe Makini sana na Usalama wako, Mji huu ni hatari zaidi nyakati za Usiku
6.Mji Guatemala, Guatemala.
- Huu ni mji mkuu wa nchi ya Guatemala huko America ya Kati, Ugomvi mkubwa zaidi katika mji huo ni masuala ya madawa ya Kulevya, Makundi ya wakabaji, wezi, na wale majambazi wanaoteka Mabasi ni jambo la kawaida sanaa katika mji wa Guetemala, Ukifika katika nchi hii Unaambiwa nenda miji yote ila Usiende Guatemala, maana kuna umafia wa nje nje.
5.Acapulco, Mexico
- Mji mwingine hatari zaidi kuishi duniani Ni Acapulco uliopo nchini Mexico , Mji huu unawafanyabiashara wengi wa madawa ya kulevya, watu wa mataifa mengi huingia Mexico kufanya Biashara ya madawa ya kulevya , na vita kubwa iliyopo katika mji huu hutokana na biashara hiyo hiyo. Jiji hili linatajwa kama moja kati ya miji inayoongoza kwakuwa na kiwango kikubwa cha mauaji duniani. katika watu 100,000 watu 142 huuwawa kihalifu.
4.Baghdad , Iraq
Moja kati ya miji ambayo haushauriwi kuthubutu kwenda Baghdad nao Umo, ni mji ambao milio ya mabomu, Bunduki ni kawaida sana, Raia kama wa Marekani walishazuiliwa kabisa kwenda Mji Huo, Ni unamatukio ya kinyama karibu kila wakati, Tanzania ukiona Moshi unaweza ukajua kuna Uchafu unachomwa ila Baghdad ukiona MOSHI ujue tayari Bomu limeshafanya yake
3.Kabul, Afghanstan
Ukiwa Kabul unakuwa kama uko jeshini vile kusikia mlio wa Risasi, Bomu ni wakati wowote ule, ni mji ambao amani yake Haionekani kutokea KESHO wala Kesho kutwa, ni mji ambao ugaidi na matukio ya Kigaidi ni kawaida sana. Kidunia Upo nafasi ya Tatu kwenye miji hatari zaidi
2.Karachi, Pakistan
Ni Mji unaokabiliwa na Matatizo na Ugomvi unaotokana hasa na masula ya kisiasa, Utekaji, Kujitoa MHANGA, Bunduki ni nyumbani kwa huu Mji wa Pakistan, Kutokana na hali hii watalii wengi hawashauriwi kwenda katika mji Huu, na umekuwa kati ya mji wenye watalii wachache zaidi dunaini kutokana na hali ya amani kuwa mbaya
1.San Pedro Sula,Honduras
Ni Mji ambao umekuwa Ukiripotiwa kuwa na mauji kwa muda mrrefu sana katika miji yote Duniani, Kuuana katika Mji huu ni kawaida sana unaambiwa katika vifo vya watu 100,000 169 wote hufa kwa Vifo vya Kushambuliana kati ya watu, usafirishaji wa Vifaa vya Kijeshi kama Bunduki Unatajwa kama chanzo kikubwa hali inayopelekea Karibu kila Raia kumiliki kifaa cha moto
0 comments:
Post a Comment