Hamidu Bobali (Kushoto), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CUF Taifa (JUVI CUF) akizungumza na waandishi wa habari leo.
JUMUIYA ya Vijana ya Chama cha CUF (JUVICUF),
Profesa Ibrahim Lipumba kutothubutu kufanya ziara katika mikoa ya
Kusini kwani atajikuta akidhalilishwa na kuendelea kukosa heshima zaidi
katika jamii, anaandika Charles William.
Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa hapa nchini, ingawa tayari chama hicho kimetangaza kumfukuza uanachama kwa tuhuma za kufanya vitendo vilivyo kinyume na Katiba ya CUF.
Hamidu Bobali, Mwenyekiti wa
JUVICUF Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, amesema vijana wa CUF
hawatakubali Prof. Lipumba na wapambe wake wajaribu kuzunguka katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Lindi na Mtwara ili kukivuruga chama hicho.
Mbele ya wanahabari leo,
jijini Dar es Salaam, Bobali ameeleza kuwa Jumuiya ya Vijana wa chama
hicho (JUVICUF), inaunga mkono maamuzi yote halali yaliyotolewa na
mamlaka halali za chama ambalo ni Baraza kuu la Uongozi la
Taifa ikiwemo ya kusimamishwa na kuwafukuza baadhi ya wanachama wake 11
ambao wanaenda kinyume na taratibu za chama.
‘’CUF ni chama cha kupigania
haki hivyo abadani hakitayumbishwa na njama mbalimbali zinazoendelea za
kutaka kututoa nje ya ajenda za kudai haki, pia ni taasisi kubwa ambayo
inaamini katika jitihada za kudai haki. Wakati njama za kutuhujumu
zikiendelea, jitihada za kudai haki zanzibar, zimefikia sehemu nzuri na
baadhi ya ushahidi jamii imeanza kushuhudia,’’ ameeleza Bobali.
Bobali amewataka vijana wote
wa CUF nchini, kutotoa ushirikiano wowote kwa maadui wa chama ambao
wanatarajia kuanza ziara wiki ijayo katika mikoa ya Kusini, Lindi,
Mtwara na Tanga katika lengo lilelile la kuweka mpasuko ndani ya chama.
“Wana lengo la kukivuruga na
kukidhoofisha chama na wanataka kuvuruga ushirikiano na vyama vingine
vya Ukawa, sisi kama vijana tupo imara, hatutaruhusu hilo litokee,
tutawakabili na kwa hakika hawatofanikiwa katika hilo,” amesisitiza Bobali.
Naibu Katibu wa JUVICUF ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia amesema Abdul
Kambaya, aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
kabla ya kusimamishwa uongozi katika chama hicho, ndiye anayeongoza
zoezi la kuchochea vijana wakipinge chama kutokana na kukosa nafasi ya
kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni analoliongoza baada ya kumuangusha katika kura za maoni Julai mwaka jana.
Kwa upande wake Juma Kombo,
Mbunge wa Jimbo la Wingwi, Pemba ambaye pia ni Afisa Haki za Binadamu
(JUVICUF), amesema CUF Zanzibar ipo imara huku wakiwataka vijana wa
Zanzibar kutoyumbishwa na watu wachache wanaotumika kukihujumu chama hicho
0 comments:
Post a Comment