Askofu wa Jimbo la Moshi, Isaac Amani.
Moshi. Askofu wa Jimbo la Moshi, Isaac Amani amewataka wazazi kuacha kufanya mauaji kwa kutoa wanafunzi mimba pamoja na wao wenyewe na kwamba hali hiyo ni ukatili uliokithiri wa kuua watu na kuangamiza Taifa.
Askofu ameyasema hayo leo kwenye ibada takatifu ya kuwaombea wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mitihani yao mwanzoni mwa Novemba mwaka huu iliyoenda sambamba na Jubilee ya miaka 25 ya shule ya sekondari Sangiti, Kibosho mkoani Kilmanjaro.
Amesema kutoa mimba ni kuua uumbaji wa Mungu aliyetoa zawadi kwa mwanadamu na kwamba wanawake wakifanya mauaji hayo ambayo yamekithiri kwa kasi nchini kwa kutumia maneno ambayo yanamchukiza mwenyezi Mungu kwa uumbaji wake.
0 comments:
Post a Comment